Miss Tanzania Kuvalishwa Taji la Milioni 6 Kichwani

Miss Tanzania Kuvalishwa Taji la Milioni 6
Shindano la kumsaka mrembo wa Tanzania Maarufu kama Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika September 8 mwaka huu ambopo  ndiyo siku ya tukio lenyewe na watakaofika ukumbini wataweza kumuona Malkia mpya wa Bongo akivikwa ‘milioni 6 kichwani’

New Miss Tanzania 2018 si tu kwamba utafanyika kwenye ukumbi wa hadhi ya juu, bali tukio zima litakuwa katika ufahari wa kipekee.

Kabla hujaenda ukumbini utakuwa unafahamu namba ya kiti chako na mahali kilipo ukumbini (Hata uchelewe hakai mtu), na mambo yote yatakuwa kwenye utaratibu wa kipekee.

Viingilio: V.V.I.P itakuwa 150,000 (laki na nusu), V.I.P 100,000 na Ordinary (kawaida) ni 70,000 (elfu 70).

Basilla ambaye anaongoz jeshi la uandaaji Miss Tanzania, amesema: “japokuwa kwenye mashindano ya Dunia hakuna kipengele kinachomlazimisha mrembo kuwakilisha utamaduni wa nchi yake, sisi tutahakikisha tunaitangaza nchi yetu na vivutio vyake”



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad