Mke wa Mzee Majuto Atimuliwa Kwenye Nyumbani kwa Mumewe

Mke wa Mzee Majuto Atimuliwa Kwenye Nyumbani kwa Mumewe
Mke wa marehemu Mzee Majuto anaripotiwa kuondoka nyumbani kwa mume wake jijini Tanga na watoto wake huku ikidaiwa kuwa sababu kubwa ya yeye kurudi nyumbani kwao jijin Dar ni kutokana na maneno aliyoambiwa na watoto wake wakubwa kuwa hawana uwezo wa kumlea mpaka arobaini.

Mwanamke huyo ambae alikuwa bega kwa bega na mzee majuto kwa kipindi chote cha uhai wake na ugonjwa wake mpaka anafariki, alikuwa mke wa pili wa mzee majuto na alibahatika kuwa na watoto nae huku mzee majuto akiwa na watoto wengine wakubwa aliozaa kabla ya kumuona mke huyo aliyepo sasa.

Hata hivyo inadaiwa kuwa mama huyo pamoja na kwamba alikuwa na watoto walikuwa wakisoma jijini Tanga, imemlazimu kuondoka na watoto hao na kuwaacha shule.

Baada ya kumtafuta moja ya watoto wa marehemu Mzee majuto alikiri na kusema kuwa ni kweli mama yao hayupo amerudi Dar lakini aliwaaga kuwa anakwenda nyumbani kwao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad