Mkongwe Chuji Anarudi VPL “Ukijua Tuliza Mpira na Kutoa Pasi inatosha”

Star wa zamani wa vilabu vya Simba nanYanga Athumani Idd ‘Chuji’ msimu wa 2018/19 tutamuona tena ligi kuu Tanzania bara akiwa na timu ya ‘wagosi wa kaya’ Coastal Union kutoka Tanga.

Coastal Union tayari imeingia kambini kujiandaa na ligi kuu, miongoni mwa wachezaji waliowahi kuingia kambini ni mkongwe Chuji ambapo kambi ya timu hiyo ipo maeneo ya Kange nje kidogo ya jiji la Tanga.

Chuji amezungumzia mambo mbalimbali kuelekea msimu mpya wa ligi kuu.

Usajili wa Coastal Union

Kwa wachezaji waliosajiliwa tukikaa na kushirikiana tutafanya kazi vizuri.

Msimu wa 2018/19 kutakuwa na timu 20 ambapo kila timu itacheza mechi 38, Chuji ni mzoefu wa ligi anaona msimu utakuaje?

“Ligi ya timu 20 itakuwa na changamoto nyingi, lazima wachezaji tuwe fit, tukiwa fit tutaweza kufanikisha malengo ya timu. Mechi 38 si mhezo kama hatutakuwa fit ligi itakuwa ndefu.”

Coastal Union imechanganya wachezaji wazoefu na vijana, Chuji anaamini timu itafanya vizuri.

“Kwa mchanganyiko uliopo kwenye timu tutapambama kuhakikisha tunatetea kinachowezekana ndani ya Coastal. Hatutaki kushuka kama maandalizi yetu tutakuwa na maandalizi mazuri tutamaliza kwenyenafasi nzuri.”

Muda mrefu hajaonekana ligi kuu, wadau wa soka wamtarajie Chuji yupi?

“Kwa Tanzania wamtegemee Chuji yuleyule, waangalie kutakuwa na mabadiliko gani yatakuwa yamekuja. Wanasema, ukijua kutuliza mpira na kutoa pasi inatosha, mengine yanakuja tu. Kujengwa kisaikolojia tunaingiaje kwenye ligi kwa sababu msimu uliopita tulicheza ligi daraja la kwanza.”

“Tunaingia msimu wa ligi kuu, mimi naijua ligi kuu inamaana ushindani utakuwepo, lazima tuoneshe ushindani kwa vijana.”

Watu wanamsema sana Chuji

“Mambo ya kusemwa yameanza tangu miaka hiyo, bora uangalie yako usisikilize ya mtu. Kama kusemwa ingekuwa unatoboka, mimi mwili mzima ungekua na matobo.”

Ana kiwango cha kurudi tena Taifa Stars?

Sijui, lakini kwanza ngoja nitetee timu yangu.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad