Mkurugenzi TWAWEZA Afunguka Kuhusu Kupeleka Passport Yake Uhamiaji

Mkurugenzi TWAWEZA Afunguka Kuhusu Kupeleka Passport Yake Uhamiaji
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TWAWEZA, Aidan Eyakuze amedai kuwa Idara ya Uhamiaji inashikilia hati yake ya kusafiria ambapo amezuiwa kusafiri kwa kutumia Shahada ya Dharura iliyotolewa kwa utaratibu uliopo ili aweze kushiriki mikutano ya kikazi kwenye Ofisi za TWAWEZA jijini Nairobi nchini Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Twaweza, Eyakuze, amesema hadi sasa bado hajajua sababu ya msingi juu ya Idara ya Uhamiaji kuishikilia hati yake ya Kusafiria(Passport), na hakuna taarifa yoyote ya amri ya kimahakama yenye kuidhinisha jambo hilo.

“Kwa wiki kadhaa sasa TWAWEZA, imekua katika changamoto kubwa ya mashirikiano baina yake na baadhi ya Taasisi za Serikali kufuatia uzinduzi wa taarifa za ripoti mbili za Sauti za Wananchi mnamo July 5, 2018 zenye vichwa vya habari visemavyo “Kuwapasha viongozi” na “Nahodha wa Meli yetu wenyewe” -Aidan Eyakuze

“Ni zaidi ya miaka 8 sasa tangu Shirika hilo lianzishwe mnamo mwaka 2009, ambapo limefanya kazi za tafiti mbalimbali na miongoni mwa tafiti zao zimeweza kuishtua serikali katika ufatiliaji wa masuala muhimu hususani katika sekta ya elimu,” amesema Eyakuze
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad