Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa Mwandishi wa habari aliyepigwa na polisi wakati akitekeleza majukumu yake katika Uwanja wa Taifa ulioko jijini Dar es Slaam alikuwa mbishi na alimkaba Askari polisi akitaka kuingia sehemu ambayo imekataliwa kuingia, ndipo askari wakawa na hasira na kuanza kuvutana ndipo ugomvi Ukaanza.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati akiwasili jijini Arusha kwa ziara yake ya kutembelea eneo la Mto wa Mbu ambapo yalitokea matukio ya wanawake kubakwa na kuuawa ,ziara ambayo inalenga kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo hayo ikiwa ni kuimarisha ulinzi na kuongeza idadi ya polisi.
Sirro amesema kuwa katika tukio la kupigwa mwandishi wa habari kuna uchunguzi unafanyika ambapo baadae wataelezea ukweli baada ya kukamilisha.
Amesema kuwa mwanzo inaonekana mwanahabari alifanya vurugu na jalada lazima lifunguliwe pamoja na askari polisi waliokuwa wanampiga upelelezi utafanyika ili kuchukua hatua kwa sababu kila jmbo linataka upelelezi.
Amesema kuwa Mwanahabari alivua shati mwenyewe na kuanguka chini kisha kukimbia mbele kwenye kioo cha camera ili kuonekana amepigwa jambo ambalo siyo sahihi.