Mkuu wa Mkoa wa Njombe Awataka Watumishi wa Halmashauri Kurudisha Milioni 41 Ndani ya Siku 15

Mukuu wa Mkoa wa Njombe Awataka Watumishi wa Halmashauri Kurudisha Milioni 41 Ndani ya Siku 15
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka, amewataka watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Makete waliotumia vibaya fedha za miradi ya maendeleo wilayani humo zaidi ya milioni 41 zirudishwe kabla ya tarehe 30 mwezi huu.


Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.

Ole Sendeka, ametoa agizo hilo katika kikao cha madiwani wa halmashauri hiyo na kujadili hoja za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambapo amewataka madiwani kusimamia na kuhoji fedha za miradi ya maendeleo ili kuwezesha fedha hizo kufanya kazi kama zilivyokusudiwa.

Katika mkutano huo kubwa lililoibuka ni upotevu wa miradi ya Afya katika halmashauri hiyo ziliztolewa kwa msaada wa shirika la kuhudumiwa watoto Duniani UNICEF, Shilingi milioni 41 ambapo baadhi ya wataalamu wamehusishwa na upotevu huo.

“Licha ya baadhi ya fedha kuokolewa na TAKUKURU lakini kuna baadhi ya fedha zinatakiwa kutolewa majibu ya kina juu ya matumizi yake lakini mpaka ifikapo tarehe 31 wawe wameshaziridisha fedha hizo”, amesema Ole Sendeka.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka madiwani kujenga utamaduni wa kuwahoji wataalamu kuhusu fedha za miradi mbalimbali ya halmashauri.

June 9, 2017  wakati akifungua semina ya mtandao wa wabunge wa Afrika walio katika mapambano ya rushwa (APNAC) tawi la Tanzania, Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa alisema serikali imefanikiwa kuokoa Sh bilioni 53.9 kutokana na uchunguzi na operesheni mbalimbali zilizofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika mwaka 2016/2017.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad