Aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa amefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo.
Mkwasa yuko jijini New delhi, India ambako amefanyiwa upasuaji huo mkubwa na imeelezwa bado yuko katika chumba cha usimamizi maalum, yaani ICU.
“Kweli Mkwasa amefanyiwa upasuaji wa moyo nchini India. Alikwenda kule akiambatana na mkewe Betty Mkwasa,” alisema mmoja wa ndugu wa familia ya Mkwasa.
Awali, wakati akieleza alitaka kujiuzulu Yanga, Mkwasa alisema hali yake kiafya haikuwa nzuri. Wengi waliona kama alitaka kukimbia matatizo kwa kuwa klabu hiyo ilikuwa ikiandamwa na ukata.