Moise Katumbi, kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, amezuiwa kurudi nchini kugombea urais katika uchaguzi mkuu Desemba mwaka huu.
Serikali ya Congo imemzuia Gavana huyo zamani wa jimbo la Katanga anayeishi uhamishoni Afrika kusini kurudi nyumbani.
Katumbi aliomba ruhusa kuingia nchini leo asubuhi kuwahi kuwasilisha makaratasi yake ya uteuzi wa chama kuwa mgombea urais kwa tume ya uchaguzi nchini.
Sababu za Moise Katumbi kuanzisha Chama akiwa Afrika Kusinihttps://www.bbc.com/swahili/medianuai/2016/03/160308_katumbi
Maafisa wa polisi huko Lubumbashi wameweka vizuizi katika bara bara kuu na usalama umeimarishwa ndani na katika maeneo yalio karibu na uwanja wa ndege.
Kuna mipango ya kuzifunga njia za ndege kutua kuizuia ndege ya Katumbi isitue DRC.