Mshiriki wa michezo ya video aua watu wawili kwa risasi Marekani

Mshiriki wa michezo ya video aua watu wawili kwa risasi Marekani
Polisi nchini Marekani inasema kuwa mshiriki katika michezo ya video kwenye mji wa Jacksonville mjini Florida amewaua watu wawili kwa kuwapiga risasi.

Takribani watu wengine 14 wamejeruhiwa katika tukio hilo.

Mtuhumiwa huyo ambaye pia amefariki, amejulikana kwa jina la David Katz mwenye miaka 24 ambaye anatokea Baltmore na alisafiri mpaka Florida kwa ajili ya mashindano hayo.

Polisi inasema upelelezi zaidi unaendelea juu ya sababu halisi ya Katz kufanya mauaji hayo.

Sehemu ambayo tukio hili linatajwa kutoke
Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema Katz alichukua hatua hiyo baada ya kushindwa katika michuano hiyo ambapo baadae alijiua mwenyewe.

Hata hivyo polisi imekataa kuthibitisha taarifa za Katz kupandwa na hasira na baadae kuua kwa sababu ya kushindwa katika mchezo ambao alikua anaupenda.

Nini kilitokea?

Kwa nini Wakenya wameorodheshwa kuwa wahamiaji wenye bidii zaidi nchini Marekani?

Wachezaji walikua wakiendelea na mashindano katika sehemu moja maarufu ya michezo ijulikanayo kwa kifupi GLHF wakati risasi za moto zilipoanza kusikika Jumapili mchana.

Milio mingi ya risasi inaweza kusikika katika mkanda wa video ambao baadhi ya watu waliurekodi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad