Msukuma Kama Zitto Kabwe, Atoa Jimbo Lisilo lake


Hata hivyo, Mbunge huyo alitua katika jimbo ambalo siyo la kwake, kama ilivyotokea kwa Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe ambaye aliingia matatani hivi karibuni kwa kosa la kuhutubia mkutano katika jimbo la Kilwa Kusini.

"Ardhi hii ina neema ya kutosha, naombeni mlime mazao mbalimbali kwani mna uwezo wa kuilisha nchi nzima,   hivyo epukeni uvivu jishughulisheni," alisema.

Akizungumza na wakazi wa Kata ya Migungani katika kampeni za udiwani juzi, alisema ni vizuri wakalima kilimo cha umwagiliaji.

Alisema kama tatizo ni maji atalifikisha suala hilo kwa viongozi wa juu ili ufumbuzi upatikane kwa wakati muafaka.

Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso, alisema serikali ipo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake.

Alisema CCM inahitaji maendeleo na hata bajeti zilivyokuwa zikijadiliwa na wabunge wa upinzani, zilikuwa zikipinga kuleta maendeleo kwa wananchi.

"Nyie wenyewe ni mashahidi kipindi cha bunge, CCM ilisema maendeleo yao yanatoka nje ya bunge na kusema maandamano, sasa makosa ni ya viongozi wenu mlio watuma kuwawakilisha bungeni," alisema.

Kumekuwa na matatizo mengi kwa upande wa elimu ikiwemo Shule ya sekondari ya Migungani, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknologia na Mafunzo ya Ufundi, William ole Nasha, alisema serikali imejipanga kutatua changamoto hizo na anajipanga kutembelea shule hiyo siku za karibuni.

"Nafanya jitihada za kila namna nikiwa kama mlezi wa jimbo hili kuhakikisha changamoto hiyo inatatulika, ikiwemo kumalizika kwa vyumba vya madarasa, ofisi na nyumba za watumishi, lakini pia serikali imetenga Sh. milioni 700 kwa ajili ya kukarabati chuo cha FDC.

Aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Monduli, mwaka 2015, Namelok Sokoine, alisema kwa sasa maendeleo yanahitajika katika jimbo hilo.

Aliwataka wakazi wa Kata ya Migungani kumchagua diwani wa CCM ili akayasemee matatizo yao kwa wakati.

Alisema uchaguzi wa mwaka ule, wengi walichukuliwa na mafuriko na sasa wametambua wapi walikosea wakaamua kurudi kwenye chama chenye amani, weledi na utiifu hivyo tuwapokee kwa upendo.

Aliongezea Chadema ilichuka kata 13 kwa udiwani kati ya kata 20 zilizopo jimboni hapa, na CCM ilichukua kata saba lakini madiwani wa Chadema wamegundua kuwa walikosea na sasa wamerudi karibu wote na Chadema imebaki kata nne tu lakini nao wapo njiani kurudi CCM.

"Ndugu zangu, siwezi waficha mkichagua upinzani maendeleo mtayasikia kwa wengine, tuchagulieni Benedict Mawala, akaisemee kata hii, na hata tukaiongoze halmashauri yetu, tusikosee tena," alisema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad