Mtoto mchanga wa kike aliyezaliwa akiwa ameota jino moja ameng'olewa jino hilo akiwa na siku 12.
Mama wa Isla-Rose Heasman, Jasmin kutoka Plymouth Devon nchini Uingereza, alisema ''hakutegemea'' kuwa angempeleka binti yake kwa daktari wa meno katika umri mchanga.
''Ilibidi atolewe jino, ilikuwa inaogopesha.Alikuwa jasiri kuliko mimi, hakulia kabisa,''Alieleza
Kituo hicho cha tiba ya meno kimesema kuwa Isla-Rose ni ''mgonjwa mwenye umri mdogo zaidi'' kuwahi kutokea, na alipatiwa beji kama zawadi
Watoto wengi huota meno wanapofikia umri wa miezi sita wengine wakiwa na miezi na wengine mpaka baada ya mwaka mmoja.
Isla-Rose alipatiwa dawa ya kumkinga na maumivu kabla ya kutolewa jino, alipatiwa zawadi kwa kuwa alikuwa jasiri
''Ilinibidi nitoke nje ya chumba nikiwa nalia kwa sababu sikuweza kuvumilia kutazama mwanangu akiwa katika maumivu.