Museveni Atishia Kuivunja Tume ya Uchaguzi na Kutaka Kuunda Mpya Ikiwa na Makada Kutoka Chama Chake

Museveni Atishia Kuivunja Tume ya Uchaguzi na Kutaka Kuunda Mpya Ikiwa na Makada Kutoka Chama Chake
Rais Yoweri Museveni ameapa kuivunja Tume ya Uchaguzi iliyopo sasa akidai inakula rushwa na kwamba ataunda mpya ikiwa na makada kutoka chama chake cha NRM.
“Tume ya Uchaguzi imejaa watu waliooza,” shirika la utangazaji la NTV lilimnukuu Rais Museveni akiwaambia wanawake katika kongamano lililofanyika Jumapili.
“Nitawaondoa (EC). Kwa nini tusumbuliwe na maofisa wala rushwa wa tume ya uchaguzi wakati NRM ina nguvu kazi ya kutosha? Lazima waondolewe. Watoke,” alisema katika kongamano la Baraza la Taifa la Wanawake.
Hata hivyo, katika taarifa rasmi iliyotolewa Jumapili jioni, Ikulu haikueleza chochote kuhusu tishio la Museveni kuivunja EC.
Taarifa hiyo ilimnukuu Rais akiwaambia viongozi wa wanawake kuinua elimu na uwezeshaji kiuchumi.
Onyo la Museveni limekuja siku chache baada ya NRM kuangushwa katika uchaguzi mdogo wa ubunge katika Manispaa ya Arua uliofanyika Agosti 15 ambapo upinzani ulishinda licha ya yeye mwenyewe kuweka kambi kumnadi mgombea wake wa chama Nusura Tiperu.

Chaguzi ndogo
Machi, Paul Mwiru wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) alimshinda Nathan Nabeta wa NRM katika jimbo la Jinja Mashariki.
Juni, mgombea wa NRM Winfred Masiko aliangushwa na Betty Muzanira wa FDC katika mbio za kuwania kiti cha wanawake wilaya ya Rukungiri.
Julai, Asuman Basalirwa kutoka chama cha Jeema, alishinda kiti cha Manispaa ya Bugiri baada ya kuwaangusha wapinzani wake akiwemo Francis Oketcho wa NRM.
Akizungumzia sababu za chama chake kushindwa katika chaguzi hizo, Museveni alisema NRM ilipoteza Jinja Mashariki kwa sababu inadaiwa upinzani ulisafirisha wapigakura kutoka nje ili wampigie Mwiru.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad