Mwanachama wa Chadema mbaroni kwa kumjeruhi kada wa CCM


JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia mmoja wa wanachama wa Chadema kwa tuhuma za kumjeruhi kada wa CCM aliyefahamika kwa jina moja la Idd baada ya kuibuka kwa vurugu kati ya makundi mawili. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Ramadhan Ng'anzi amesema tukio la vurugu hizo zimetokea leo kati ya saa nne na saa tano asubuhi eneo la Mianzini. 

Amefafanua Polisi waliwahi kufika eneo la tukio na kufanikiwa kuzima vurugu hizo na kumkamata anayetuhumiwa kujeruhi na anahojiwa, huku aliyejeruhiwa naye amepatiwa matibabu. 

Alipoulizwa jina la anayetuhumiwa kujeruhi Kamanda Ng'anzi amejibu kwa sasa yupo nje ya ofisi yake kwa ajili ya kufuatilia na kuangalia hali ya usalama na hasa kwenye kata zinazofanya uchaguzi unafanyika unaofanyika leo. 

Hata hivyo inaelezwa kada aliyejeruhiwa ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kaloleni mkoani Arusha. 

Kuhusu hali ya usalama amesema Mkoa wa Arusha hali ni tulivu na amani imetawala katika maeneo yote yakiwamo ya kata ambazo yanafanya uchaguzi na kwamba hata vurugu ambazo zilizotokea ni kwenye kata ambayo haina uchaguzi. 

"Arusha hali ni shwari mno.Hakuna vurugu na watu wanaendelea na shughuli zao.Hata katika kata ambazo kunafanyika uchaguzi mdogo kuko shwari na mambo yanakwenda vizuri,"amesema Kamanda Ng'anzi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad