Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Akamatwa na Polisi Kwa Kujiunga na Kikundi cha Ukabaji


DODOMA: Jeshi la Polisi linamshikilia Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Itega, Mohamed Ramadhani(18) kwa kujiunga na kikundi cha uhalifu cha 'Kamchape' ambacho kinajihusisha na ukabaji
-
Kamanda wa Polisi, Gilles Muroto amesema kijana huyo amekuwa akijishughulisha na uhalifu ambapo kwa siku za hivi karibuni aliwahi kukiri kumkaba mama yake mzazi lakini mama huyo hakujua kuwa aliyemkaba ni mwanaye
-
Aidha, Kamanda Muroto amesema baada ya tukio hilo kijana huyo aliachiwa lakini alikamatwa tena, alipobainika kuwa amehusika katika kuvunja nyumba ya mtu na kuwafunga kamba wenye nyumba ili wawaibie
-
Kwa upande wake mtuhumiwa huyo amedai chanzo cha yeye kujihusisha na matukio hayo ya uhalifu ni kutokana na hali ngumu ya maisha ndio imemfanya kutenda hayo
-
Wengine waliokamatwa ambao wanaunda kundi hilo la Kamchape lililopo Kizota ni Abdul Mchangala(18), Mashaka Idd(17), Salum Mohamed(24) na Hamis Kikweli(40)
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad