Mwanamke mwenye asili ya Tanzania amekuwa wa kwanza wa asili ya Afrika kuteuliwa kuwa mbunge nchini Pakistan, na kutoa matumaini kwa watu wa jamii ndogo na maskini nchini humo yenye asili yake Afrika.
Tanzeela Qambrani, 39, aliteuliwa na chama cha Pakistan People's Party (PPP), cha waziri wa zamani Benazir Bhutto kuhudumu katika kiti kilichotengewa wanawake kwenye bunge la mkoa wa Sindh kusini mwa India.
Ana matumaini kuwa uteuzi wake baada ya uchaguzi wa mwezi uliopita utasaidia kuondoa unyanyapaa ambao umekuwepo dhidi ya jamii ya Sidi, jina wanaloitwa watu wa asili ya Afrika wanaoishi maeneo ya pwani ya Makran na Sindh nchini Pakistan.
"Kama jamii ndogo iliyopotelea kwenye jamii kubwa za wenyeji, tumekuwa na wakati mgumu kudumisha mizizi yetu ya Afrika na tamaduni, lakini ningependa kuona kuwa jina Sidi linakuwa lenye heshima," Bi Qambrani ambaye mababu zake walitokea Tanzania aliiambia BBC.
Mwanamke huyo aliapishwa Jumatatu wiki hii na amenukiliwa na mtandao wa The News International akisema kwamba alijihisi kama Nelson Mandela.
Watu wengi wa jamii ya Sidi walitokana na watumwa waliopelekwa India kutoka Afrika Mashariki na Wareno.
Wanahistoria wanasema mababu zao walikuwa pia wanajeshi, wafanyabiashara, madereva na mahujaji wa Kiislamu.
Niliambiwa you are rafiki wa kipakistani kwa mara ya kwanza kuwa kuna watu watu weusi kama mimi waishio kwao Pakistan. Nikaenda ku Google na nilipata mshtuko ambao sijausahau nilipoona picha za watu hao. Bila maslezo immediately nilitambua hawa ni ndugu zangu wa damu na ni watanzania. Nikamwabia yule mama wa kipakistani, huyu ni ndugu yangu Nikamwabia hata tukipima DNA inasema hivyo, nikajikuta nalia. Nikasevu ile picha kwenye simu yangu. Mtoto niliyemwonau alikuwa anadhabihiana na picha za watoto wa kaka zangu na mimi mwenyewe nilivyokuwa mdogo. Nilimwambia yule mpakistani najisikia guilty tumewatelekeza. Kisha nikarudi tena ku Google, nikaona ni kweli wanatokea Africa ya Pwani ya Tanzania hadi kusini yay Tanzania. Mpaka Sasa naamini yule mtoto ni ndugu yangu halisi. Bibi yangu naye alikamatwa utumwa, kwa bahati alinusurika, hakuendelea na msafara wa watumwa. Ndiio na mimi nikazaliwa Tanzania kama matokeo. Wanatusimulia nyakati hizo unaweza uende tu shambani kutafuta chakula na usirudi nyumbani, unakamagwa na kutekwa na watekaji. Watu waliishi kwa hofu kuu. Hata babu yangu pia alitekwa utumwani. Utumwa ulikuwa ni janga kuu nyakati hizo, nahisi kama janga la ukimwi kwa sasa. Ukinusurika ni jambo tu la kumshukuru mwenyezi Mungu.
ReplyDeleteNaomba ubalozi wa Tanzania Pakistan umtumie pongezi maalum mama huyu, naye atajisikia vizuri mno. Mwambie tupo wote. Pia bw mahiga kana inaruhusiwa mwandiikie kaujumbe. Hata raisi Magufuli ukiweza naomba umwandikie Mwambie wote tumefurahi we are so pride of her
ReplyDelete