Mwanasheria wa Rais TRUMP Afikishwa Mahakamani

Mwanasheria wa TRUMP afikishwa mahakamani
Mwanasheria wa zamani wa raisi Donald Trump amefikishwa mahakamani na kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya fedha za umma na uvunjifu wa sheria za uchaguzi katika mahamakamya New York, ambapo hivi karibuni alikiri kuhusika na miamala ya fedha kwa mcheza filamu za ngono aliyekuwa na uhusiano na raisi ili kumziba mdomo.

Michael Cohen amekata rufaa katika mahakama ya Manhattan dhid ya madai juu yake kwamba alikiuka sheria za uchaguzi, na kudai kuwa alifanya hivyo kwa uongozi wa "mgombea", kwa lengo la kupisha uchaguzi salama.

Michael Cohen alikuwa chini ya uchunguzi maalum kutokana na tuhumza zilizokuwa zinamkabili za kuweko uwezekano wa udanganyifu dhidi yake juu ya masuala ya benki na ushuru.

Mamlaka ya shirikisho la Marekani lilikamata hati kutoka katika ofisi ya Cohen mnamo mwezi Aprili mwaka huu,kufuatia uchunguzi uliohumsisha mshauri maalumu Robert Mueller.

Anahusishwa na tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi wa na nafasi ya uraisi na ambao mpaka sasa umewagusa watu wapatao thelathini .

Uchunguzi huo mpaka sasa ume kwisha baini makosa matano, chanzo cha madai hayo hakijajulikana dhahiri mpaka sasa na hii haina maana kwamba bwana Cohen anakwenda kinyume na raisi Donald Trump.

Katika kipindi cha miaka kumi ya utumishi wake kama mwanasheia wa raisi, Cohen anatuhumiwa kuandaa malipo kwa mwigizaji wa senema za ngono , Stormy Daniels, mnamo mwaka 2016.

Mnamo mwezi wa tano mwaka huu, raisi wa Marekani alikiri kumpa pesa Cohen za malipo ya kutaka kumnyamazisha mwigizaji Stormy Daniels kuhusiana na suala la kuwa na mahusiana na mlimbwende huyo siku kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo.

Ingawa siku za hivi karibuni raisi Trump amekana kufahamu muamala wa malipo ya dola za kimarekani laki moja na selathini kama sehemu ya malipo ambayo hayajabainishwa.

Mwezi uliopita imefahamika pia kuwa bwana Cohen alimrekodi kwa siri raisi, wakati walipokuwa wakijadiliana ununuzi wa haki za umiliki mcheza filamu za ngono wa kulipwa mlimbwende Karen McDougal ikiwemo hadithi yake kutoka kwa kampuni dada la jarida la kitaifa la Enquirer.McDougal aliuza taarifa zake kwa jarida hilo wakati wa kampeni za uraisi.

Malipo yafanywayo kwa siri kwa niaba ya mwanasiasa ama mgombea yeyote yanaweza kuchukuliwa kama ukiukwaji wa sheria za kampeni za nchini Marekani.

Mwanasheria wa msanii huyo ambaye kwa pamoja anawashtaki raisi Trump na Cohen ameandika katika ukurasa wake wa twitter kuwa maamuzi ya leo yanaweza kumsaidi kushinda kesi yake dhidi ya raisi Trump.

Kama ilivyo ada ya raisi Trump, kutoa matamko kupitia ukurasa wake wa twitter, mpaka sasa hajaandika chochote kuhusiana suala hilo, ambaye kwa sasa yuko West Virginia. Kwenye ratiba zake za mikutano ya kisiasa,

Katika kesi ingine ya pili, iliyokuwa ikiendelea mjini Virginia, mahakama imemkuta na hatia ya mashtaka kumi na nane kutokana na udanganyifu wa kodi na masuala ya ki benki kampeni meneja wa raisi Donald Trump, Paul Manafort.

Lakini pia mahakama hiyo haijaafiki makubaliano juu ya mashtaka mengine kumi ambayo hakimu ametangaza wazi kuwa mbaya.

Bwana Manfort kwa muujibu wa tuhuma zinazomkabili anaweza kukabiliwa na kifungo cha muda mrefu gerezani.Rais Donald Trump ameonesha kusikitishwa kwake kutokana na hukumu hiyo lakini uchunguzi uliofanyika ni kama ulikuwa unamtafuta mchawi.

Raisi Trump alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza na katika mkutano wa hadhara huko West Virginia.Akiwa mjini humo rais amewaambia waandishi habari wazi kuwa anajisikia vibaya kutokana na yanayomkuta Paul, na kwamba kesi hiyo haina uhusiano wowote na kile kinachodaiwa udukuzi wa Urusi. Mwishoni mwa wiki iliyopita alimsifu Paul Manfort kuwa ni mtu mzuri na kwamba wanachomtendea inasikitisha na mwanzoni mwa wiki hii aliishutumu timu ya Robert Muller kwa kufurahia uangamizaji wa maisha ya watu na kuwaita wanaoaibisha taifa.

Mahakama pia imetoa muda mpaka tarehe 29 mwezi huu ili kujiridhisha ikiwa hakuna sababu ya kufungua mashtaka mapya dhidi ya uamuzi iliyoutoa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad