Nimevumilia vya kutosha hii tabia sasa naona itakua imefika kikomo.
Naishi na mpenzi wangu hatujafunga ndoa tatizo nashindwa kumuelewa kila siku niendapo kazini na kurudi jioni lazima nimuachie elfu kumi na tano 15,000/-kusudi nikirudi jioni nikute mezani kumependeza nadhani mmenielewa cha ajabu jamani nakuta ugali na dagaa akibadili sana tembere kaomba kwa jirani
Huu ni ungwana jamani? kumuambia nashindwa naona kama takua naingilia mambo ya jikoni ambayo hayanihusu na nisipokula huo ugali ananuna, pia kesho yake nisipo acha hela nikirudi hatuongea mnuno mwanzo mwisho
Sielewi nifanyeje na Nilikuwa nafikiria Kumuoa