Najiona Mwenye Bahati Sana Maana Haya Maisha Ninayoishi Sijawahi Kuyaota- Harmonize

Najiona Mwenye Bahati Sana Maana Haya Maisha Ninayoishi Sijawahi Kuyaota- Harmonize
Msanii wa muziki nchini Tanzania, Harmonize amedai kuwa katika maisha yake hajawahi kufikiria kuishi maisha yenye mafanikio makubwa kama anayoyaishi kwa sasa.

Harmonize amesema kuwa miaka mitano iliyopita alikuwa mtu wa kawaida na alikuwa akifanya biashara ndogo ndogo maarufu kama Machinga Kariakoo jijini Dar es salaam lakini kwa sasa amepiga hatua kubwa kimafanikio kwenye muziki.

“Miaka (5) iliyopita nilikuwa nafanya biashara za kudunduliza maeneo haya ya #Kariakoo kwa lugha nyengine nilikuwa #Machinga shida, tabu, shuruba, nilizokuwa nikizipitia , M/mungu peke ndie anayefahamu..!! Hata wimbo wangu wa #Matatizo 90% umebeba uhalisia wa maisha yangu sana. Sina utajiri wowote ila afadhali niliyoipata najihisi ni mwenye bahati  Sana.“ameandika Harmonize kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya kutembelea marafiki zake wa miaka ya nyuma katika mitaa ya Kariakoo.

“Maana maisha ninayoishi sikuwahi hata kuyaota, Nimshukuru M/mungu kwa kunipa Nafasi hii ya kukumbuka Ndugu zangu ambao nimewaacha katika, Eneo hili na kupata nafasi ya kuzungumza nao mawili ,matatu Ya kuwapa Moyo, faraja, Mungu anawaona na Maombi yangu yapo kwenu sitochoka Kuwa nanyi siku zote…!!! Na kidogo Au kingi changu kiwafikie kama fadhila ambazo ni ngumu Kuwafikia watu wote..!!! Ila nyie Mliobahatika kwa leo mkawe wawakilishi wa wengine M/mungu awabariki sana…!!! Ndugu zangu Changamoto, pandashuka, majaribu, zifanye kuwa motisha wa kukufanya uongeze juhudi…!! #MunguHajakuumbaUjeteseka..!! Ipo siku.“amemaliza Harmonize.

Harmonize ni moja ya wasanii ambao kwa sasa Afrika Mashariki wanafanya vizuri sana kwenye tasnia ya muziki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad