Nandy Awatolea Povu Wanaosema Anabebwa Kwenye Muziki

Nandy Awashukia Wanaosema Anabebwa Kwenye Muziki
Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kama Nandy amewatolea povu zito watu ambao wamekuwa wakimtuhumu Nandy kwa kubebwa Kwenye Muziki.


Nandy amefunguka kuzungumzia kelele ambazo zipo kwenye mitandao ya kijamii kwamba anabebwa kwenye muziki wake na sio kipaji chake ambacho kimemfikisha sehemu aliyofikia.

Kwenye Interview aliyofanya na Bongo 5, Nandy amedai anashangazwa na tuhuma za kubebwa kimuziki Wakati anaimba nyimbo na zinapigwa kila kona  na zinashika chati kama kawaida:

Hayo maneno ya watu hayanipi tabu yoyote kwa sababu each and everyday nasikia kuhusu kubebwa kubebwa lakini nyimbo zangu zinahit redioni na zinapigwa mpaka mikoani na zinatrend Kwenye chati kwa mfano kama sasahivi ‘ninogeshe’ ina viewers milioni 5 kwaiyo suala la kubebwa halipo”.

Lakini pia Nandy amedai yeye kama staa kuongelewa ni jambo la kawaida kwani ukiwa msanii halafu ukaona hakuna hata mtu mmoja anakuongelea basi wewe sio staa.

Tuhuma Za Nandy kubebwa zilianza kutokana na Nandy kuimba nyimbo nyingi za wasanii wa zamani Lakini pia Nandy amewahi kukiri kuandikiwa nyimbo zake nyingi anazoimba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad