Nay Wa Mitego- Nipo likizo ya Mapenzi, Nasuburi Nipate Mwanamke Anayejielewa Nimuoe

Nay wa Mitego amekanyaga nyoka? Akiona jani anashtuka? Amesisitiza kwa sasa yupo mwenyewe (singo) anasubiri apate mwanamke anayejielewa ambaye atakuwa na uhusiano naye na hatimaye kufunga naye ndoa.

‘’Unajua mimi nina watoto lazima niwe na mtu ambaye anajua kuwa mimi nawapenda watoto wangu, pia watoto wangu watainjoi kuwa naye lakipi sitaki kutaja sifa za mwanamke ninayemtaka wasije wanawake wakajipanga wakajitengeneza’’

‘’Kuna wakati unaona kabisa watoto wangu wanahitaji kuwa na mama ambao ni mama yao kabisa lakini hata familia inakutaka kuoa’’

Hivi karibuni Nay Wa Mitego aliachana na aliyekuwa mpenzi wake aitwaye Nini na amekiri kuwa yeye ndio chanzo cha kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Nini, lakini mpenzi wake huyo hakutaka melewano akasepa!

‘’Mahusiano yangu na aliyekuwa mapenzi wangu wa sasa Nini yalitokea yametokea bahati mbaya, najua kosa ni la kwangu na yeye hakuwa mwelewa, hakutaka maelewano akaondoka’’

‘’Kwa wanawake niliozaao nao hatukupanga kuoana, kwa sasa nipo singo nimeamua kuwa mwenyewe mpaka siku nitakapoamua kumpata mwanamke ambaye nitamuoa’’

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad