NEC yaviasa vyama vya siasa kufuata sheria za uchaguzi


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevikumbusha vyama vya siasa nchini na wadau wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, miongozo na maelekezo yote kipindi cha uchaguzi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage alipokuwa akitangaza tarehe ya uchaguzi na zoezi la kuchukua fomu za uteuzi ambapo litakuwa Septemba 7 hadi 13 mwaka huu, ambapo uteuzi wenyewe utakuwa Septemba 13, 2018 huku akitaja tarehe ya kuanza kampeni kuwa ni Septemba 14 hadi 12 Oktoba mwaka huu.

Ametangaza tarehe rasmi ya uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Liwale Mkoa wa Lindi mara baada ya kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge kuwepo wazi kwa nafasi hiyo ambapo siku ya uchaguzi huo imepangwa kuwa Oktoba 13 mwaka huu.

“Tume inavikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, miongozo, na maelekezo yote wakati wa kipindi cha uchaguzi huo mdogo,”amesema Jaji Kaijage.

Aidha, uchaguzi huo wa marudio umekuja mara baada ya kujiuzulu kwa Mbunge jimbo la Liwale kupitia tiketi ya chama cha Wananchi (CUF), Zuberi Mohamed Kuchauka, ambaye alijiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kumfanya apoteze sifa ya kuwa Mbunge na kulifanya jimbo hilo kuwa wazi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad