Nedy Amkingia Kifua Ruby ishu ya Kuzidiwa na Madawa ya Kulevya


Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Neddy Music amefunguka na kumkingia kifua mwanadada Ruby kuwa tokea alipoanza kumfahamu na kufanya naye kazi, hajawahi kumuona akijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya kama baadhi ya watu wanavyompakazia kwenye mitandao ya kijamii.


Nedy amebainisha hayo leo Agosti 20, 2018, alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha 'PLANET BONGO' kinachorushwa na East Africa Radio baada ya kuulizwa swali kwamba, hakuhofia kufanya kazi na Ruby kutokana na 'skendo' zake za uteja.

"Nilimshirikisha Ruby katika wimbo wangu wa 'one and only' kutokana na kuufahamu uwezo mkubwa wa kufanya vizuri licha ya Ruby kuwa kimya kutokana na mambo mengi yaliyokuwa yanaendelea nyuma yake. Tangu nimekaa na Rubby na kusafiri naye zaidi ya mikoa minne, sijawahi kumuona au kumkuta na chochote ambacho anakitumia kama watu wanavyodai",amesema Nedy.

Aidha, Nedy amedai kwamba, haitotokea yeye kushawishika na makundi ya watu anaozunguka nao kila uchao, kumuingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya kwa kile alichoeleza kuwa amelelewa kwenye maadili ya kutosha ndani ya familia yake.

Itakumbukwa mnamo Juni 22, 2018 mwanadada Ruby alikanusha kuhusu picha zilizokuwa zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha akiwa amekonda mpaka mbavu kuomekana na kusababisha jamii kumuhusisha na utumiaji wa vilevi vikali pamoja na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad