Mkali Wenu ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha PLANET BONGO 'PB' kinachorushwa na East Africa Radio, baada ya kupita miezi kadhaa tangu Ebitoke kumkana hadharani kuwa hamtambui kwa chochote kile na kuzua maswali mengi baina ya watu wawili hao.
"Laiti mimi nisingezaliwa na kuamua kuingia kwenye uchekeshaji basi leo hii asingefahamika Ebitoke, Bwana Mjeshi hata mama Ashura kwa sababu wamekuja baada mimi kuwepo na 'idea' zangu za 'video clip' fupi za uchekeshaji mitandaoni ambazo nilienda kuzitambulisha katika kampuni ya Timamu na wao ndio wakatambulika kupitia kazi zangu hizo. Ila sikushangaa kwa Ebitoke kunikana kwasababu ndivyo binadamu tulivyo", amesema Mkali wenu.
Mbali na hilo, Mkali Wenu amesema hana uhakika wowote wa mrembo huyo kumiliki nyumba kama anavyo jinadi huko mitandaoni na sehemu nyingine.
"Sijui kama kweli Ebitoke ana nyumba lakini ngoja tu nicheke kinafiki maana hilo ndio lina jibu tosha kuhusu Ebitoke", amesisitiza Mkali wenu.
Miaka kadhaa iliyopita msanii Mkali Wenu alikuwa miongoni mwa wachekeshaji walioweza kutikisa mitandao ya kijamii, kwa video zao fupi fupi na kujizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa watu mbalimbali.