Niva Atoa Wosia Mzito "Naomba Kuzikwa na Steve Nyerere"

Niva Atoa Wosia Mzito "Naomba Kuzikwa na Steve Nyerere"
Msanii wa bongo movies Niva amefunguka na kutoa wosia wake na kusema kuwa anaomba endapo atakufa basi msanii Steve Nyerere ashughulikie mazishi yake,Niva ambae siku hizi ameonekana kujigamba na kuongea kwa kujiamini mbele za watu amesema kuwa kwake haina shida na anatamani sana katika mazishi yake yasimamiwe na Steve Nyerere.

Niva anasema kuwa hata  kuna watu wanamsema vibaya na kusema anakula rambi rambi kwake wala hakuna shida ilimradi azikwe kwa heshima kama vile ambavyo Steve amekuwa akijituma kufanya kazi hiyo.

Hata hivyo niva amelaani vikali wale wanaomwita na kumsema Steve nyerere vibaya  na kuwaita wapuuuzi na hawajui wanachokiongea.

Kumekuwa na maneno ya kejeli ya muda mrefu , baadhi ya wasanii wanamsema vibaya Steve Nyerere na kusema kuwa amekuwa akijihusisha katika misiba kwa ajili ya kula pesa za rambirambi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad