Nyerere Amuibukia Jokate Kisarawe


Katika hali ambayo haikutegemewa Steve Nyerere ndiye msanii pekee maarufu  aliyejitokeza katika shughuli ya kuapishwa kwa mkuu mpya wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo.


Kutokana na umaarufu wa Jokate  na kushiriki mara kadhaa kwenye Muziki, filamu na mchango wake mkubwa katika jamii. watu wengi walitegemea katika shughuli ya kuapishwa  kwa mkuu huyo wa wilaya ya kisarawe iliyofanyika mjini Kibaha kungekuwepo na wasanii na watu wengi maarufu wangehudhuria lakini cha kushangaza Steve Nyerere pekee ndiye aliyenaswa na kamera za wanahabari.

Baada ya waandishi kumuona Steve walimkimbilia kwa ajili ya kumuhoji sababu za yeye kuwepo kwenye shughuli hiyo pekee yake, ambapo amejibu “ kwanza nimekuja kuungana kwa sababu ya familia ya pande zote mbili, Zainabu Kawawa ni mtu wangu wa siku nyingi sana tangu akiwa mbunge alikuwa akisapoti wasanii kwa namna moja ama nyingine  (Zainabu ni mkuu mpya wa Wilaya ya bagamoyo naye ameapishwa leo) na Jokate ni moja ya fungu letu”.

Ameongeza “ Sitaki kusemea kwa nini wengine hawajaja nataka kusema kwamba hata wengine ambao hawajaja inawezekana wengine kutokana na hali ya sasa hivi kila mmoja anahangaika lakini nimekuja kuwakilisha kwa niaba ya wenzangu kuhakikisha kwamba Jokate asijisikie mpweke kwamba wasanii wenzake tumelipokea hili na tunaamini Jokate hatotuangusha wasanii wenzake”.

Steve Nyerere ameongeza kuwa anaimani kwamba Jokate atakwenda kuitangaza ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo walizunguka  nchi nzima kuhakikisha inatimizwa kwa kuwatendea haki watanzania na kuleta maendeleo kwa taifa.

Akijibu swali kuhusu utendaji kazi wa Jokate, Steve amesema “ kwanza akafanye kazi ambayo ametumwa na Mh Rais, akatangaze Ilani ya Chama cha Mapinduzi lakini pili ahakikishe anasimamia haki ya wananchi wa Kisarawe, akasimamie ukusanyaji wa kodi na mapato ni mtu ambaye anauwezo ana fikra anasababu na mbunifu hakika wana-Kisarawe wamepata mtu”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad