IKIWA ni saa chache baada mtu asiyejulikana kusambaza taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba msanii wa filamu nchini, Jenifer Kyaka maarufu ka Odama amefariki dunia, msanii huyo ameibuka na kutoa kauli nzito kwa mtu aliyetenda jambo hilo.
Odama amesema inaonyesha mtu aliyemfanyia hivyo ana chuki binafsi na kusema anatambua kama ipo siku itafika atakufa kwani kila nafsi itaonja mauti huku.
“Kifo kipo na hakuna atakaekikwepa, kila binadamu ataonja mauti na kukamilika kwa maisha yetu hapa duniani. Lakini pia hata kama humpendi mtu unamchukia iwe alikutendea ubaya au umeamua tu kumchukia sio vizuri kumuombea kifo tena ukaona haitoshi basi unaweka matangazo mitandandaoni.
‘Nakushukuru wewe ulieamua kufanya hili, najua unaniongezea umri wa kuishi, na nikuambie tu kua mimi ni mzima wa afya na ninaishi kwa kudra za Mungu. Nitakufa tu pale siku yangu itakapofika mungu atakapoamua kunichukua lakini sio kwa kutaka wewe.
“Sijui nilichokukosea mpaka kufikia kunitangazia kifo. Nakuombea maisha marefu ili uendelee kuniona nikivuta pumzi ya mungu. Binadamu sisi laiti tungelijua kua si kitu kabisa tungeacha chuki zisizo na sababu. Asante mungu kwa kila kitu,” ameandika Odama.
Jambo la kuzushiwa vifo kwa mastaa na viongozi maarufu limekuwa likikithiri siku hadi siku, ikumbukwe kwamba enzi za uhai wake, Mzee Majuto aliwahi kuzushiwa kifo mara kadhaa na yeye kukanusgha, wengine ni Mzee Agustiono Mlema na wengine jambo ambalo si la kiungwana.