Ofa ya Kuinunua Arsenal yakubaliwa

Wamiliki wa Arsenal Stan Kroenke na Alisher Usmanov
NA ELBOGAST MYALUKO
Mmiliki wa asilimia 30 ya hisa ndani ya klabu ya Arsenal Alisher Usmanov amekubali ofa ya Paundi milioni 600 zaidi ya shilingi trilioni 1 aliyotoa tajiri Stan Kroenke, ambaye ni mmiliki mwenza wa Arsenal kwaajili ya kununua asilimia hizo 30 Alisher Usmanov.

 Mapema leo Agosti 7, 2018 Alisher Usmanov alitangaza kuziweka sokoni hisa zake huku  Kroenke anayemilikia asilimia 67 ya hisa akitangaza nia ya kutaka kuzinunua asilimia 30 ili aimiliki moja kwa moja klabu hiyo kupitia kampuni yake ya KSE.

Usmanov amesema kuwa amevutiwa na mpango wa KSE ambao ni kuifanya Arsenal kuwa ya ushindani zaidi na kutwaa mataji kama EPL na ligi ya mabingwa Ulaya sambamba na kuwekeza kwenye timu ya wanawake na timu za vijana hivyo yupo tayari kumuuzia  Kroenke ili alitekeleze hilo.

Pamoja na matajiri hao kuonekana kukaribia kukubaliana lakini mashabiki wa timu hiyo ambao nao ni moja ya wamiliki wa hisa 'Arsenal Supporters Trust' (AST), wamepinga vikali hatua ya timu hiyo kumilikiwa na mtu mmoja wakiamini kuwa utakuwa ndio mwisho wa wanachama hao kumiliki hisa ndani ya timu yao.

Kroenke mwenyewe amesema kuimiliki Arsenal peke yake kutasaidia utekelezaji wa mambo kwa wepesi kwani hakutakuwa na pingamizi na klabu pia itakuwa na uwezo wa kununua wachezaji wakubwa na wenye ushindani kwani hatapenda kuona biashara ya kampuni yake KSE inafeli.

EATV
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad