Okwi Awatumia Salamu Kagera Sugar

Okwi Awatumia Salamu Kagera Sugar
MABAO mawili yaliyofungwa na Mganda Emmanuel Okwi yaliwafanya mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Arusha United katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa jana,-

ikiwa ni mechi ya mwisho kwa Wekundu wa Msimbazi hao kabla ya kuivaa Mtibwa Sugar Jumamosi.

Okwi alifunga bao la kwanza katika dakika ya saba akimalizia pasi ya Asante Kwasi, huku Ali Kabunda akifanikiwa kuisawazishia timu yake hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza dakika 10 baadaye akitumia makosa yaliyofanywa na mabeki wa Simba katika eneo la 18.

Bao la pili la Okwi lilipatikana katika dakika ya 29 na kuwafanya mabingwa hao wa Bara kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1 kwenye mchezo huo ambao ulihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Simba ilikosa bao la wazi katika dakika ya 42 baada ya Hassan Dilunga kupiga shuti pembeni na kupoteza pasi aliyopewa na Okwi, lakini kiungo huyo aliyetokea Mtibwa Sugar alilazimika kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mzambia, Clatous Chama kutokana na kuwa na maumivu yaliyotokana na mchezaji wa Arusha United.

Timu zote zilifanya mabadiliko katika kipindi cha pili, lakini hakuna upande ambao ulifanikiwa kuliona bao la mwenzake huku wachezaji wa Arusha United ambao waliahidiwa zawadi ya Sh. milioni moja kwa kila bao watakalofunga walionekana 'kuamka', hata hivyo jitihada zao hazikuzaa matunda.

Kikosi cha Simba kinatarajia kurejea Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujiandaa na safari ya kuelekea Mwanza kuwafuata Mtibwa Sugar katika mechi ya Ngao ya Jamii itakayopigwa keshokutwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Simba: Aishi Manula, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Erasto Nyoni, Pacsal Wawa, Jonas Mkude, Hassan Dilunga/ Clatous Chama (dk 44), James Kotei/Mohamed Rashid (dk 56), Meddie Kagere/ Adam Salamba (dk 72), Emmanuel Okwi/ Rashid Juma (dk 81) na Shiza Kichuya/ Mzamiru Yasin (dk 76).

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad