Pamoja na Kumfukuza Kocha Wenger...Arsenal yaendeleza Unyonge, yachapwa Nyumbani

NA ELBOGAST MYALUKO
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka ya England, Manchester City, wameanza mbio za kutetea ubingwa wao kwa kushinda ugenini dhidi ya Arsenal kwa mabao 2-1 kwenye mchezo uliomalizika usiku huu.

 Manchester City ambayo iliwaanzisha benchi nyota wake kadhaa waliokuwa katika kikosi cha kwanza msimu uliopita kama Kevin De Bruyne, Gabriel Jesus, Nicolás Otamendi na Leroy Sané ilitangulia kwa bao la Raheem Sterling dakika ya 14, kabla ya Bernardo Silva kuongeza la pili dakika ya 64.

Kocha mpya wa Arsenal Unai Emery amepoteza mechi yake ya kwanza ya ligi kwenye uwanja wa nyumbani hivyo kuanza vibaya kibarua chake ambacho amekichukua kutoka kwa Arsene Wenger ambaye alikuwa na uzoefu wa ligi kuu ya EPL kwa zaidi ya miaka 20. Katika mechi 6 za hivi karibuni Arsenal imepoteza 4 na sare 2 dhidi ya Man City.

Bao la Bernardo Silva leo, limemfanya nyota huyo kufikisha mabao matano katika mechi zake  za mwisho alizoanza. Hii imekuja baada ya nyota huyo wa Ureno kushindwa kufunga bao hata moja kwenye mechi zake 9 za kwanza ndani ya kikosi hicho.

Muingereza Raheem Sterling yeye amefunga bao lake la 50 kwenye ligi kuu ya Englanda huku likiwa bao lake la 3 kufunga nje ya boksi. Man City sasa imeungana na timu zingine kubwa ambazo zimepata ushindi kwenye mechi zake za ufunguzi ambazo ni Manchester United, Chelsea, Liverpool na Tottenham.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad