Papa Francis awasili Ireland kwa masikitiko
0
August 26, 2018
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa John Francis amewasili nchini Ireland akiwa na huzuni kubwa baada ya Kanisa hilo kushindwa kushughulikia tatizo la unyanyasaji wa kingono wa watoto unaofanywa na mapadri.
Akiwa katika Kasri la Dublin, Papa Frances amesema naye pia anahisi maumivu na aibu juu ya kushindwa kwa mamlaka ya Kanisa Katoliki kushughulikia kashfa hiyo ya kunyanyaswa kingono watoto.
"Kushindwa kwa mamlaka ya kanisa - maaskofu, wakuu wa kidini, makuhani na wengine - kushughulikia uhalifu kumesababisha hasira na bado ni chanzo cha maumivu na aibu kwa jumuiya ya Kikatoliki, "amesema Frances akiwa katika Kasri la Dublin alipokutana na Waziri Mkuu Leo Varadkar.
Francis atakutana na wahanga wa unyanyasaji wa kingoni unaofanywa na mapadri wa kanisa katoliki, wakati wa ziara yake hiyo ya masaa 36 nchini Ireland.
Ni mara ya kwanza katika kipindi cha miongo minne kwa papa wa Kanisa Katoliki kuizuru Ireland. Mamlaka ya Vatican imesema ziara hiyo itatoa fursa nyingi za kuweza kulijadili tatizo la unyanyasaji wa kingono linaloendelea katika kanisa Katoliki.
Ingawa watu 600,000 wanatarajiwa kuhudhuria Misa itakayoongozwa na Frances Jumapili, idadi hiyo ni kidogo ikilinganishwa na miaka 40 iliopita.
Zaidi ya thuluthi tatu ya idadi jumla ya watu wa Ireland ilimiminika barabarani kumuona Papa John Paul II mwaka 1979, katika wakati ambapo talaka ya ndoa pamoja na utumiaji wa njia za uzazi wa mpango vilikuwa ni vitu visivyoruhusika nchini humo.
Leo hii, Ireland sio tena nchi inayoongozwa kwa misimamo ya Kikatoliki, na katika miaka mitatu iliyopita wapiga kura wameidhinisha utoaji mimba pamoja na ndoa za jinsia moja kupitia kura za maoni, hatua zote zikiwa ni kinyume na mafundisho ya madhehebu ya Kikatoliki.
Idadi ya watu wataokakusanyika barabarani au kuungana na Papa Frances katika sala ya pamoja, inatarajiwa kuwa robo tu ya watu milioni 2.7 waliompokea John Paul II mwaka 1979.
Hali hiyo inaashiria jinsi gani ufuasi wa Kanisa Katoliki umepungua, tokea kudhihirika kwa visa vya unyanyasaji wa kingono kwa watoto katika miaka ya 1990.
Tags