Polepole Awacheka Vyama vya Upinzani Asema Watapata Tabu

Polepole Awacheka Vyama vya Upinzani Asema Watapata Tabu
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa viongozi wa vyama pinzani watapata tabu kwakuwa wanashindwa kusimama katika itikadi zao na kuhitaji huruma kwa wananchi.

Polepole amefunguka hayo kupitia Weekend BreakFast leo Jumamosi Agosti 4, 2018 ya East Africa Radio ambapo amesema kuwa wapinzani wanashindwa kutimiza wajibu wao na kusimamia migogoro ndani ya vyama vyao, matokeo yake wanasingizia kuonewa na CCM.

''Kusema wanaotoka upinzani kuhamia CCM, wananunuliwa ni kutafuta huruma, mwaka 2010 Mawaziri wakuu wastaafu wawili (Edward Lowasa na Frederick Sumaye) waliondoka CCM lilionekana ni jambo jema ila leo wanapokuja kwetu linakuwa jambo baya huo ni unafiki wa kisiasa'', amesema Polepole.

Polepole ameongeza kuwa hakuna mbunge anayenunuliwa kuhamia CCM ila ukweli ni kwamba akitaka kuunga mkono juhudi za Rais hawezi kuunga akiwa upinzani lazima atakuwa mnafiki ndio maana wanaenda CCM ili wawe huru.

Mpaka sasa jumla ya wabunge wanne kutoka vyama vya upinzani wamekwisha jiunga na CCM wakiwemo watatu kutoka Chadema na mmoja kutoka CUF huku Madiwani wakiwa zaidi ya 50 wamejiunga na CCM.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad