JESHI la polis limeeleza sababu za kumkamata Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini,Esther Matiko na wafuasi wake 16 akiwemo mwandishi wa habari wa Gazeti la Tanzania Daima,Sitta Tuma wakiwa kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi unaoendelea ndani ya kata ya Turwa ya halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara jana kwenye viwanja vya mkuyuni kuwa ni kukiuka sheria ya uchaguzi ya mwaka 2015.
Akiongea na mwaandishi wa habari kamanda mkoa wa kipolisi Tarime/Roreya,Henry Mwaibambe amesema kuwa jeshi la polis linamshikilia Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini,Esther Matiko Chadema na mwandhishi wa habari wa Gazeti la Tanzania Daima,Sitta Tuma na watu wengine 16 kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.
Mwaibambe aliongeza kuwa polisi walipokea barua kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi kata ya Turwa,Peter Julius ikiwataka kwenda kusimamisha mikutano ya kampeni ya Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kwa siku Nne kuanzia Agosti,08 hadi Agost,11,2018 kutokana na sababu ya kukiuka kifungu cha sheria ya Taifa ya uchaguzi.
"Tulipokea barua kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi kata ya Turwa,Peter Julius ambayo ilikuwa ikitutaka jeshi la polisi kwenda kusimamisha mikutano ya kampeni ya Chadema kuanzia Agosti,08 hadi Agosti,11,2018 na kuwa chama cha NCCR Mageuzi pamoja na Chama cha mapinduzi wao wataendelea na kampeni za kuwanadi wagombea wao"alisema Mwaibambe.
Kamanda huyo pia alisema kuwa kuhusiana na mwandishi wa habari kukamatwa alikuwa sehemu ya mkutano na hakuwa sehemu ya kutekeleza majukumu yake kwasababu alikaririwa na kupigwa picha za video akiwa sehemu ya mwanaharakati sio kama mwandishi wa habari.
Kamanda Mwaibambe ameongeza kuwa bado polis wanafanya kazi yao pindi watakapokamilisha kazi ya upelelezi watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili.
Kwa upande wake katubu wa Chama cha Demkorasia na maendeleo Chadema mkoa Mara,Chacha Heche alisema kuwa wao hawana taarifa yoyote ya kuwa mikutano yao imezuiwa na ndio sababu walikuwa wamejiandaa kwenda eneo la mkutano ndipi walishitukia polis wanakuja na magari na kuanza kutawanya wasikilizaji kwenye mkutano kituo cha Mkuyuni kata ya Turwa.