Producer Abbah Ajibu Tuhuma za TID

Producer Abbah Ajibu Tuhuma za  TID
Mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva nchini, Abbah Process amefunguka na kudai, sio kweli muziki wa sasa umejawa na unaiNigeria mwingi bali watu wanashindwa kutofautisha kati 'sound' hizo pindi wazisikiapo masikioni mwao.


Abbah ametoa ufafanuzi huo kupitia kipindi cha PLANET BONGO kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV kila siku ya Jumapili kuanzia saa 12:00 jioni, baada ya mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Khaleed Mohamed ‘TID’ kudai bongo flava imejaa unaiNigeria mwingi na kuacha uhalisia wake.

"Ni kweli TID anaweza akawa amesikia hivyo kutokana na uwelewa wake lakini tunajua kwamba muziki ambao waliokuwa wamezoea kaka zetu sio huu ambao upo kwa sasa. Tunajaribu kufanya 'sound' ziwe za kiafrika nasio za kiNaigeria, nadhani watu wanashindwa kutofautisha kati ya Nigeria na Afrika", amesema Abbah.

Pamoja na hayo, Abbah ameendelea kwa kusema "muziki umeshabadilika na kubadilika huko kuna weza kuwafanya kaka zetu wakisikia kama 'sound' za Nigeria. Sisi tunajaribu kufanya muziki ambao unaenda sawa na soko la dunia na wala hatuna haja ya kukopi kwa watu wa Ulaya".

Muziki wa bongo fleva umekuwa ukipigiwa kelele muda mrefu na wadau mbalimbali wa tasnia hiyo, kuwa unapoteza uhalisia wa neno bongo fleva kutokana na wasanii kupenda kuimba tamaduni za nchi nyingine na kuacha kukuza za kitanzania ili kusudi hao wa nje kuiga za kwetu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad