Mkuu wa mkoa wa Tabora AGGREY MWANRI amewaagiza wakuu wa wilaya zote za mkoa huo kufanya ukaguzi kwenye nyumba zote ambazo zinadaiwa kutumika kama madanguro kwa ajili ya kufanyia biashara haramu ya ngono ambapo inadaiwa baadhi ya wanawake wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa kubadilishana na magunia ya mpunga.
Ametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa kampeni maalumu ya upimaji wa VVU ijulikanayo kama Furaha yangu iliyofanyika rasmi katika viwanja vya parking wilayani Nzega.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa wilaya nao wanakiri kuwepo kwa biashara hizo na kwamba tayari wamejipanga kuzidhibiti.
Gunin kamba ni mganga mkuu wa mkoa wa Tabora anabainisha hali ya maambukizi ya VVU ilivyo hadi sasa mkoani hapa.