Unatamani kusikia ngoma mpya kutoka kwa Rihanna? Huwenda mrembo huyo akawa amerejea tena studio kutengeneza wimbo mpya kwa ajili ya masikio yetu.
Kupitia Insta stories Rihanna ameonekana akiwa studio ya nyumbani tayari kufanya kitu kwa mashabiki zake.
Msanii huyo hajaachia wimbo wowote tangu 2016 alitoa album yake 'ANTI' huku tukishuhudia mwaka jana akionekana kushirikishwa kwenye ngoma mbili ikiwemo 'N.E.R.D' ya Lemon na 'Wild Thoughts' ya DJ Khaled.
Mapema mwezi uliopita taarifa kutoka mtandao wa Rolling stone ziliripoti kuwa Rihanna anatayarisha album mbili kwa mpigo (Reggae & Dancehall) na (Pop & RnB) huku ikidaiwa kuwa kuna ngoma 500 zipo tayari chini ya watayarishaji na waandishi mbali mbali.