Robert Mugabe Amtumia Mtoto wake wa kike Kuondoa Lawama


Harare, Zimbabwe. Kiongozi wa muda mrefu nchini Zimbabwe Robert Mugabe Jumapili hakuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Emmerson Mnangagwa kuwa rais badala yake alimtuma binti yake Bona na mumewe kuwakilisha familia hiyo.

Taarifa ya Instagram kutoka kwa Mugabe inasema hakuhudhuria sherehe hizo kwa kuwa alikuwa hajisikii vizuri na kwamba mkewe hakuwepo.

Mnangagwa aliapishwa Jumapili kuwa Rais wa Zimbabwe siku mbili baada ya Mahakama ya Katiba kutupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wake iliyokuwa imefunguliwa na muungano wa upinzani wa MDC ambao mgombea wao Nelson Chamisa alidai kuibiwa kura.

Chamisa alilalamikia hukumu hiyo ya Ijumaa iliyotoa mwanya kwa Mnangagwa kuapishwa.

Mugabe alisema awali kwamba atahakikisha anamchagua mpinzani Nelson Chamisa akidai kwamba yeye ndiye mwenye haki ya kuliongoza taifa hilo.

Mugabe na mkewe Grace walionekana hadharani wakipiga kura tangu kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 kujiuzulu nafasi ya urais kufuatia shinikizo kutoka kwa jeshi na raia.

Baadhi ya raia wa nchi hiyo wakiwemo viongozi wa kimataifa na wanadiplomasia walihudhuria sherehe ya kuapishwa Mnangagwa katika uwanja wa michezo wa mjini Harare.

Muda mfupi kabla ya kuapishwa taasisi ya kimataifa ya Marekani inayohusika na masuala ya demokrasia ilisema vyama vya siasa havikutendewa haki na watu hawakuruhusiwa kupiga kura kwa njia huru.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad