Nyota wazamani wa timu ya taifa ya Brazil, Ronaldo amelazwa hospitali ya Ibiza kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa pneumonia.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 41 ameripoti kupitia mtandao wake wa twitter kuwa amefikishwa hospitalini hapo siku ya Ijumaa na kutarajia kupata ruksa leo siku ya Jumatatu.
Ronaldo amefunga jumla ya mabao 62 akiwa na timu yake ya taifa ya Brazil yakiwemo magoli mawili aliyoifunga Ujerumani kwenye mchezo wa fainali ya kombe la dunia mwaka 2002.
Nyota huyo wazamani wa klabu za Real Madrid, Barcelona, Inter Milan pamoja na AC Milan amewashukuru mashabiki zake kwa kumtakia afya njema.
Ronaldo ameshinda mataji mawili ya La Liga akiwa na Real na Uefa Cup akiwa na Inter.
Amekuwa sehemu ya kikosi cha Brazil ambacho kimetwaa taji la kombe la dunia mwaka 1994 na kuiwezesha timu hiyo kufika fainali mwaka 1998.
Lakini pia amewahi kutwaa taji la Ballon d’Or mara mbili mwaka 1997 na 2002.