Rosa Ree Awapa Makavu Wanaomsema Kuhusu Staili Yake ya Kubinua Mdomo

Rapper wa kike Tanzania ambae anafanya vizuri kwenye game la ndani na nje ya nchi Ambae ame hit na goma ya Marathon aliofanya na Billnas na siku mbili nyuma alisikika kwenye ngoma na Fid q inayoitwa Ole Chiza msanii Rosa Ree amedai kuwa Rapper wengine wa tanzania wakifanya vizuri yuko tayari kufanya nao kazi  ila hayuko Tayari kufanya kazi na mtu asiefanya poa.

Ameendelea kuwachana wale wanaomfatilia kuhusiana na kubinua midomo na kutoa ulimi wakati anaimba ambapo imekuwa kama ni style yake katika kila nyimbo anayotoa au kushirikishwa.

" Hawanilipii bili na kubinua kwangu midomo na kutoa ulimi sasa hivi nina super market, nimefanya kolabo na wasanii wa kimataifa zaid ya mmoja na bado nafanya vitu vikubwa mimi mawazo ya watu hazijiandiki usoni kwangu wala hazilipi bili zozote ingekuwa hela ningejali" Ameyatamka Rosa Ree

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad