Sababu ya wanawake kutotumia uzazi wa mpango yatajwa


Wataalamu wa afya wamesema jitihada za kutoa elimu ya uzazi wa mpango zinakabiliwa na changamoto ya kibajeti baada ya serikali kutenga bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 14 na kutoa shilingi bilioni mbili tu hali iliyongia upungufu mkubwa wa watoa huduma wenye uwezo na kusababisha asilimia 62 ya wanawake kutotumia uzazi wa mpango hapa nchni. 

Wakizungumza na vyombo vya habari,meneja wa  utetezi wa mradi wa uzazi wa mpango kutoka shirika la kimataifa la uzazi wa Mpango-AFP- Bwana James Mlali asema asilimia sita ya wanawake kote nchini wanatumia njia za asili na asilimia 32 wanatumia Njia za kisasa za uzazi mpango na kuitaka serikali kuweka nguvu za kutosha ili iweze kufikia azma ya kufikia asilimia 45 ya Wanawake watumie uzazi wa mpango ifikapo mwaka 2020. 

Akielezea kuhusu umuhimu wa uzazi wa mpango katika kukuza uchumi wa viwanda, afisa utetezi na tathimini wa mradi wa huduma yauzazi wa mpango amesema idadi kubwa ya wanawake hapa nchni hawashiriki katika shughuli za kiuchumi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda kutokana na kuelemewa ulezi wa familia kubwa hali inayowababishia kukosa fursa za kujiendeleza kielimu na kiuchumi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad