Saudi Arabia Yamtimua Balozi wa Canada na Kusitisha Biashara na Uwekezaji wa Nchi Hiyo

Saudi Arabia Yamtimua Balozi wa Canada na Kumuita Balozi Wake
Saudi Arabia imesema kuwa inasitisha biashara na uwekezaji wowote mpya na Canada kwa kuwa inaingilia masuala ya ndani ya taifa hilo la Ghuba.

Kwenye ujumbe kadhaa kupitia mtandao wa twitter wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Saudi Arabia, ilisema itamfukuza balozi wa Canada na kumuita balozi wake aliye Canada.

Hatua hii inakuja baada ya Canada kusema kuwa ina wasi wasi kutokana na kukamatwa kwa wapiganiaji kadhaa wa haki za binadamu.

Mwanaharakati wa Saudi Arabia adai kupata vitisho
Kati ya wale waliokamatwa ni mpiganiaji wa haki za wanawake nchini Saudi Arabia Samar Badawi.

Bi Badawi amekuwa akitoa wito wa kumalizika mfumo wa wanaume kuwasindikiza wanawake kila wanapokwenda.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ilisema haiwezi kamwe kukubali kuingiliwa kwa masuala ya ndani ya nchi yao.

Ilizungumzia taarifa ya wiki iliyopita ya wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Canada iliyoitaka Saudi Arabia kuwaachilia mara moja wanaharakati wa kupigania haki za wanawake.

Wizara nchini Saudi Arabia ilitaja hatua hiyo ya Canada kama shambulizi dhidi ya nchi yake ikisema kuwa sasa:

Serikali ya Canada hadi sasa haijatoa taarifa yoyote kufuatia hatua hizo za kidiplomazia za Saudi Arabia.

Kukamatwa huko ni kinyume na hatua zikizopigwa na serikali mwaka huu chini ya uongozi wake mrithi wa ufalme Mohammed bin Salman.

Alilijozolea sifa mwaka uliopita wakati alitangaza kuondolewa marufuku ya miongo kadhaa ya kuwazuia wanawake kuendesha magari.

Wanaharaki wa kutetea haki za wanawre wakiweo wale waliokuwa wamefungwa kwa kukiuka marufuku hiyo walisherehekea uamuzi huo.

Wanawake ni lazima wafuate sheria kali za mavazi, wasijihusishe na wanaueme wasio na mahusiano nao na wasindikizwe au wawe na ruhusa iliyoandikwa kutoka kwa mwanamume ambaye ni lazima awe ni baba, mume au ndugu ikiwa wanataka kusafiri ng'ambo, kufanya kazi na kupata huduma ya afya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad