Shirika la ndege la Saudi Arabia liitwalo Saudia Airline limesema litasimamisha safari zake kwenda mji wa Toronto Canada kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo.
Mambo matano marufuku kwa wanawake Saudi Arabia
Mapema waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Adel al-Jubeir alitangaza uhusiano baina ya nchi hizo mbili kuzorota.
Samar Badawi mwanaharakati maarufu nchini Saudi Arabia ambaye kaka yake anatumikia kifungo cha miaka kumi alikamatwa wiki iliyopita
Saudia pia imemfukuza balozi wa Canada nchini humo sambamba na kuondoa mabadilishano yote ya elimu yaliyokuwepo baina ya pande hizo mbili.
Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Canada Chrystia Freeland nchi yake siku zote itasimamia haki za binaadam pamoja na haki za wanawake.
Siku ya Ijumaa, Canada ilielezea kusikitishwa kwake baada ya kukamatwa kwa wanaharakati nchini Saudi Arabia, miongoni mwao akiwemo mwanaharakati maarufu Samar Badawi huku Canada ikitaka kuachiliwa kwao mara moja.
Riyadh inasema haikubali na kamwe haitakubali kuingiliwa kwa mambo yake ya ndani.
Saudi Arabia Yasitisha Safari za Ndege za Kwenda Toronto, Canada
0
August 07, 2018
Tags