Kundi la muziki linaloundwa na wasanii wanne kutoka nchini Kenya, Sautsol limeweka wazi kuwa Tanzania ni nchi ya mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine, kutokana na wingi wa makabila yaliyopo lakini wananchi wake wanaishi bila ya kubaguana.
Sautsol wameeleza hayo kupitia ukurasa wao wa Instagram, alasiri ya leo kwa ku-post 'video clip' inayomuonesha Rais Dkt. John Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kenya, kuhusu masuala ya mshikamano na umoja bila kujali makabila waliyo nayo.
Hayo yote yamekuja ikiwa zimepita takribani siku sita tangu walipotoa wimbo wao mpya unaoitwa 'tujiangalie', waliomshirikisha Nyashinski ambayo wameimba kwa lugha ya Kiswahili ambapo ndani ya wimbo huo wamezungumzia mambo mbalimbali yanayohusu makabila na vitu vingine.
"Tujiangalie tupo pamoja leo kuliko jana, sikio la kufa halisikii dawa, tuko kwa twitter tunajibizana. Michuki alisema tufungeni mikanda, ona leo twavuna tulichopanda, kura zetu zilitugawanya makabila na pesa pia tulimanga", Sautisol wameimba katika mashairi ya wimbo huo na kuongeza.
'So when your make bed oh!, you lie on it oon'. Usingizi gani tumelala tutajua hatujui 'vision' 2030 itabaki stori tujiangalie".