Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Atashasta Nditiye aliyeeleza kuwa katika udhibiti huo watashirikiana na NIDA kupitia vitambulisho vya Taifa.
Amesema kuwa mtu akitaka kusajili 'line'ya pili ya simu Kampuni za simu zitamuona na kujua kuwa tayari ana 'line' ya kwanza, hivyo lazima atajaza fomu maalum kueleza kwa nini anataka 'line' ya pili.
Aidha, Naibu Waziri amesema kuwa kabla ya mwaka huu kuisha 'line' za simu zitaanza kuuzwa kwenye maduka rasmi na mtu anayesajili atachukuliwa alama za vidole na picha yake
VIDEO: