Serikali Kusimamia Vyakula vya Kwenye Harusi na Misibani

Serikali Kusimamia Vyakula vya Kwenye Harusi na Misibani
Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imewataka watoa huduma ya vyakula kwenye mikusanyiko ikiwemo kwenye misiba na harusini wajisajili na endapo wasipofanya hivyo watafungiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Agnes Kijo, amesema, utoaji wa huduma ya chakula unapaswa kuzingatia sheria na kanuni bora za usafi ili kuhakikisha chakula kinachoandaliwa ni salama.

“Hatutaki tufikie hatua ya kufungiana biashara, kufikishana mahakamani bali tunahitaji watu wafate sheria kwa kujisajili ili watambulike na huduma wanazozitoa zizingatie usafi“, amesema Kijo.

Kijo amesema kuwa kwa sasa TFDA itakuwa na kazi ya kutoa elimu kwa watoa huduma hao ambapo watatoa muda maalum ili watu wajisajili baada ya hapo wataanza ukaguzi kwa kila halmashauri na itafikia hatua wataanza kusimamisha magari yaliyobeba vyakula ili kuyakagua.

Julai 13, akiwa ziarani jijini Mwanza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alitoa agizo kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Wizara ya Afya, Kitengo cha Afya ya Mazingira, kuangalia ni Mamlaka ipi inajukumu la kutazama vyakula vinavyoliwa kwenye maharusi, ili kulinda afya za walaji.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad