Shangwe Zatanda Kumkaribisha Bembe DRC

Shangwe Zatanda Kumkaribisha Bembe DRC
Kiongozi wa upinzani nchini Kongo, Jean Pierre Bemba amerudi nyumbani leo, baada ya kukaa kwa takribani muongo mmoja akiwa kifungoni na nje ya nchi ya Kongo.

Bemba alifutiwa mashataka hivi karibuni na mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC, aidha ameonesha wazi nia yake ya kugombea Urais nchini Demokrasia ya Kongo. Alishindwa katika uchaguzi wa mwaka 2006 dhidi ya Rais wa sasa Joseph Kabila ambaye muda wake umeisha tangu mwaka 2016, jambo ambalo bado linaleta maswali mengi kama ataogombea tena.

Kurudi kwa Bemba kunaonekana kusisimua upya na kutikisa siasa za Demokrasia ya Kongo, chama tawala tayari wametoa tamko kuwa Bemba hana vigezo vya kugombea nafasi ya urais nchini humo, kutokana na alikua mshitakiwa wa mahakama ya makosa ya jinai ICC.

Image caption
Mmoja wa wafuasi wa Jean Pierre Bemba
Vyama vimebakiwa na wiki moja ya kuwasilisha majina ya wagombea wao, na tayari chama cha Bemba kimeshamchagua kuwa Mgombea wao wa Urais, amesema kuwa atamuunga mkono mgombea yoyote kutoka upinzani.

Kwa upande wafuasi wa Rais kabila wanasema Bemba hatakiwi kugombea kwani anakiukuka Utaratibu wa katiba.

Kwa upande wa Kabila mwenyewe bado hajazungumza chochote juu ya kurudi kwa Bemba.

Makamu huyo wa Rais wa zamani amekua Ulaya kwa miaka 12 huku miaka 10 akiwa akitumikia kifungo kutokana na ukikukwaji wa haki za binaadamu ulifanywa na wafuasi wake katika nchi jirani Jamhuri ya Afrika ya kati, ambapo hivi karibuni alifutiwa mashtaka na ICC jambo lilomfanya aweze kurudi kwake nyumbani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad