Mwanamuziki mwanasiasa Bobi Wine ambaye amekuwa akizuiliwa kwa karibu wiki mbili nchini Uganda pamoja na wanasiasa wengine 32 wa upinzani wameachiliwa huru kwa dhamana na Mahakama Kuu mjini Gulu, kaskazini mwa nchi hiyo.
Mbunge huyo wa Kyadondo Mashariki ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi amepewa dhamana pamoja na wabunge wengine watatu, na watuhumiwa wengine wanane.
Washtakiwa hao wanadaiwa kuhusika katika kurushia mawe magari ya msafara wa Rais Yoweri Museveni wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Arua.
Kassiano Wadri aliyeshinda ubunge Arua ni miongoni mwa wabunge waliokuwazuiliwa.
Ziara ya Theresa May ina umuhimu gani Afrika?
'Mapinduzi ya nishati ya umeme Rwanda'
Kenyatta na Trump wataangazia nini White House?
Bw Wadri ameachiliwa kwa dhamana lakini akazuiwa kuzuru eneo bunge lake kwa miezi mitatu bila idhini ya mahakama.
Maombi ya dhamana ya washukiwa wengine 21 walioshtakiwa pamoja na Bobi Wine yatasikilizwa na mahakama baadaye leo.
Awali, taarifa zilikuwa zimesema kuwa wakili wa kimataifa aliyekuwa amepewa kazi ya kumwakilisha, Bobi Wine, amezuiwa kuingia nchini humo.
Shangwe Zatawala Uganda Baada ya Bobi Wine Kuachiwa Huru
0
August 28, 2018
Tags