Kwenye mahojiano na Global Publishers, Shilole amewataka mastaa hao wa kike kuacha maisha ya kuigiza mitandaoni ambapo wanaonekana wamependeza kwa kuvaa nywele zenye thamani ya shilingi milioni moja na zaidi huku wakiwa hawajafanya la maana litakalowasaidia maishani.
Nawasihi wasanii wenzangu wote siyo Wema na Uwoya tu, wapambane na waithamini shilingi mia moja maana unakuta mtu ananunua nywele za shilingi milioni moja na hana hata kiwanja hebu jiulize hapo angenunua mifuko ya simenti angepata mingapi, jamani wasanii wenzangu jitahidini kufanya mambo yatakayowasaidia katika maisha ya mbeleni.
Inashangaza sana kuona msanii anafariki msiba unaenda kufanyika kwa shangazi yake kwa sababu kuna nyumba nzuri, kwa nini tusijikwamue sasa hivi angali tuna nguvu ili baadaye tuwe na cha kujivunia jamani, inabidi tubadilike zama za kujianika mitandaoni na nywele za mamilioni zimepitwa na wakati”.
Lakini pia Shilole alitoa siri ya mafanikio yake iliyomuwezesha kujenga mjengo huo wa thamani:
Hii nyumba nimejenga kwa fedha nyingi ambazo mpaka sasa sijui jumla ni gharama kiasi gani maana sijajumlisha na fedha hizo nilikuwa kila nikipata hela kidogo nanunua simenti au mchanga na vifaa vingine hivyo mpaka nikae chini niangalie risiti nianze kuzijumlisha”.