Siamini Kama Aslay Amejenga Maana Hata Mimi Mwenyewe Naishi Kwenye Nyumba ya Kupanga- Beka Flavour

Siamini Kama Aslay Amejenga Maana Hata Mimi Mwenyewe Naishi Kwenye Nyumba ya Kupanga- Beka Flavour
Msanii wa bongo fleva, Beka Flavour amefunguka na kumkosoa mwanamuziki mwenzake Aslay kuwa hana uwezo wa kumiliki nyumba ya kifahari kama anavyojinadi huko mitandaoni, kwa kile alichokidai kuwa hana fedha za kumfanya aweze kukamilisha jambo hilo kwa sasa.


Beka Flavour ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha PLANET BONGO kinachorushwa na East Africa Radio, hii leo Agosti 23, 2018 na kusema anaweza kumiliki gari la kutembelea la aina yoyote kwa kuwa ni kitu cha kawaida lakini sio nyumba ya kuishi labda iwe ya kupanga.

"Siamini hadi leo kama anamiliki nyumba maana sio kitu cha mchezo. Mtu akikwambia anamiliki nyumba unapaswa umuheshimu sana 'so' tuheshimiane kwenye hilo. Sikatai kama ana nyumba lakini siamini kama ni ya kwake 'means' amejenga, maana mimi mwenyewe ninaisha kwenye nyumba ya kupanga na sio ya kwangu hilo siwezi kuficha", amesema Beka.

Pamoja na hayo, Beka ameendelea kwa kusema "Aslay ni miongoni mwa wasanii waliojitahidi kupambana na kazi zao na kufanya vizuri katika kipindi cha nyuma. Sijawahi kufikiria kwamba anatafuta kiki kwa kufanya hivyo".

Kauli kama hizo za Beka Flavour zimekuja baada ya kupita takribani siku 80 tokea msanii Aslay Isihaka ku-post picha katika ukurasa wake wa Instagram, iliyokuwa ikiomuonyesha yupo nje ya nyumba ya kifahari yenye rangi ya manjano.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad