Sikuwahi Kuolewa Ila Tunapokwenda Wanawake watakua Wananguvu Kuliko Kina Baba

Image result for anna makinda
Aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Anne Makinda ameelezea historia yake fupi ya maisha toka enzi anasoma hadi kuja kufanikiwa kuwa kiongozi mkubwa bungeni.



Mhe. Makinda amesema maisha yake yote yalikuwa bungeni na kipindi hicho amesema kuwa alikuwa na fujo sana kuliko hizi ambazo zinafanywa na baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani bungeni.
Mimi maisha yangu yote yalikuwa bungeni, mimi mwenyewe kama kuwa mtu wa fujo i was of those.. nilikuwaga backbencher nilikuwa na fujo nawambia ndugu zangu akina Tundu Lissu kuwa kwanza nyie hamuwezi kunifikia mimi,“amesema Anna Makinda.
Akielezea upande wa mahusiano Bi. Makinda amesema yeye hakuwahi kubahatika kuolewa na amewaasa wanawake waliokwenye ndoa kuwa makini sana pale wanapopata mafanikio kwani ndio kipindi cha kushirikiana karibu sana na wanaume zao ili kufika mbali.
Mimi sikuwahi kuolewa lakini nilipopata mtoto wangu, aliyenisaidia sana ni dada yangu. Kwa hiyo nikiwa shuleni tu IDM nikipata ile shilingi 20 kumi napeleka kwa dada, 10 nabaki nazo kwa hiyo toka huko nilikuwa nafanya kazi I have to survive .“amesema Bi. Makinda  na kusisitiza jambo kwa wanawake walioolewa.
Tunakokwenda najua kabisa akina mama watakuwa na nguvu zaidi kuliko akina baba, na ndio maana nawa-advice pia tujifunze kuwapenda hawa watu. Kwa sababu kama wewe ni Couple umeolewa halafu unakuwa successful kuliko mume wako, usipoweza kumeneji hiyo anaweza kukuharibia hata wewe, ni vizuri kumshirikisha ikawa ile successful yako ikawa ni part ya familia yako au  successful ya couple yenu,“amesema Anne Makinda akielezea historia yake kwenye mahojiano na TGNP Mtandao, tazama video hapa chini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad