Siwalaumu Wasanii Kususa Msiba wa Mama Yake Sugu...


NILIONA mjadala Twitter. Bahati nzuri aliyeuanzisha alini-mention. Aliwa-mention pia wasanii kadhaa. Mjadala ulihusu wasanii kutofika kwenye msiba wa mama yake Sugu.

Niliona orodha ya majina ya wasanii na michango waliochangishana. Kuna wasanii walijitetea. Niliona tweets za Wakazi na Niki wa Pili. Bado watu walishambulia kwamba muhimu ni kujitoa physically, sio financially peke yake.

Niliwaona Kala Jeremiah, G Solo, Dani Msimamo, Braton, Suma G, ShowKazi, Papii Kocha, Prof Jay, Nguza Viking na wengine kama nimewasahau. Wapo ambao hawakuwepo kwa sababu za msingi. Huwezi kuwalaumu. Wengine hata wangepata vipi muda wasingefika. Nao huwezi kuwalaumu. Ndivyo walivyo. Kuwalaumu ni kupoteza muda.

Kuna wasanii hawakwenda msibani kwa Sugu kwa kuhofia kuonekana misiba ya wapinzani (woga tu). Wengine walitabiri kiki ndogo, wakaona bora wasiende. Ila walijaa kwenye msiba wa mtoto wa Muna, kisa ni ule mvutano wa baba halisi, hivyo walijua vyombo vya habari vingejaaaa! Kiki ingekuwa kuuubwa! Ni upeo wao, huwezi kuwalaumu!

Tatizo wasanii Tanzania hawana umoja. Roma, Moni na wenzao walipotekwa, nyuma ya umoja wa wasanii waliosimama kidete alikuwepo Ruge. Wasanii wenyewe kuungana kuteteana hawawezi. Sugu alilia peke yake na Malaria No More. Clouds TV ilipovamiwa wasanii walikuwa kimya, ila waliposajiliwa Fiesta walipaza sauti.

Wasanii wa Tanzania hawajawahi kutambua nguvu yao! Wakati mwaka 2015 walitumiwa kama kiburudisho cha jukwaa la siasa, mwaka 2012, wasanii Senegal walimwondoa madarakani Rais Abdoulaye Wade na kumuingiza ofisini Macky Sall. Walifanya harakati mitandaoni na kwenye vyombo vya habari na walirekodi wimbo wa pamoja, unaoitwa Y'en Marre, yaani Tumechoka!

Wasanii wa Tanzania Hawajawahi kujua wanahitaji nini na hawajui cha kwao ni kipi. Sugu ni Father In Chief wa Hip Hop na Bongo Fleva. Alipigana mapambano makali kuifanya Bongo Fleva kuwa muziki wa kibiashara. Anapigana bungeni kutetea maslahi ya sanaa. Sugu na Zitto wamewezesha mauzo na shughuli zote za sanaa kuingia sekta rasmi. Ila wasanii hawamjui mwema wao. Huwezi kuwalaumu.

Ndimi Luqman MALOTO

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad